The Institute of Development Studies and Partner Organisations
Browse

Mazingatio muhimu: Mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Marburg nchini Rwanda, Oktoba 2024

Download (568.48 kB)
report
posted on 2024-11-12, 12:30 authored by Hugh Lamarque

Muhtasari huu unatoa muhtasari wa mambo muhimu kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Marburg (MVD) nchini Rwanda, ikijumuisha uwezo wa kitaifa wa kukabiliana na hali hiyo, miundo ya utawala wa ndani na athari za kikanda na kiuchumi. Muhutasari huu unatokana na mapitio ya haraka ya fasihi iliyopo iliyochapishwa na isiyo rasmi, ripoti za habari, utafiti wa awali nchini Rwanda na mazungumzo yasiyo rasmi na wadau wa kitaifa na kimataifa, na wale waliohusika katika juhudi za kukabiliana na ugonjwa huu.

Mlipuko huo ulitangazwa rasmi tarehe 27 Septemba 2024, likiwa tukio la kwanza la MVD nchini Rwanda. Wakati wa uandishi (14 Oktoba 2024), kumeripotiwa watu 62: Watu 15 wamekufa, watu 21 wametengwa na wanapokea matibabu, na watu 26 wameripotiwa kupata nafuu. Visa vingi vilivyothibitishwa vimekuwa kwa wafanyakazi wa afya. Visa vilivyothibitishwa vimeripotiwa katika wilaya saba kati ya 30 za Rwanda: Gasabo, Gatsibo, Kamonyi, Kicukiro, Nyagatare, Nyarugenge na Rubavu (tazama Mfano 1) Kuwepo kwa ugonjwa huo katika wilaya nyingi kunazua wasiwasi mkubwa kuhusu kuenea katika jumuiya. Juhudi za upimaji zimeongezeka, huku Wizara ya Afya ikiripoti kuwa zaidi ya vipimo 3,797 vimefanywa kufikia tarehe 14 Oktoba 2024.

Hatua ambazo Rwanda ilichukua katika mlipuko wa MVD zinatokana na miundombinu yake iliyopo ya afya ya umma na uzoefu wake wa kudhibiti majanga ya hapo awali, kama vile COVID-19 na kujiandaa kwa Ebola wakati wa milipuko ya homa ya virusi ya kuvuja damu katika nchi jirani. Mbinu hizo zinajumuisha kuimarishwa kwa vituo vya watu kutengwa, maabara zinazohamishika na uwezo wa uchunguzi wa wakati halisi ili kuimarisha juhudi za kudhibiti magonjwa. Wizara ya Afya, kwa usaidizi kutoka kwa WHO, imeanzisha Mfumo wa Kudhibiti Matukio wa ngazi mbalimbali, ikihusisha uwepo wa Timu za Kukabiliana kwa Haraka zinazofanya kazi katika ngazi za kitaifa, mikoa na vituo vya afya ili kumudu ufuatiliaji wa watu walioambukizwa na udhibiti wa visa. Data inadhibitiwa kupitia mfumo wa kielektroniki wa Ufuatiliaji na Mwitikio wa Magonjwa (e-IDSR). Juhudi za chanjo kwa wafanyakazi wa afya pia zimeanza kutumia chanjo ya majaribio ya MVD.

History

Publisher

Institute of Development Studies

Citation

Lamarque, H. (2024). Mazingatio muhimu: Mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Marburg nchini Rwanda, Oktoba 2024. Sayansi ya Jamii katika Jukwaa la Hatua za Misaada (SSHAP). www.doi.org/10.19088/SSHAP.2024.063

Series

SSHAP Brief

Version

  • VoR (Version of Record)

Copyright holder

Institute of Development Studies

Country

Rwanda

Language

SW

IDS team

Health and Nutrition

Pagination

13pp

Usage metrics

    Social Science in Humanitarian Action (SSHAP)

    Categories

    No categories selected

    Licence

    Exports

    RefWorks
    BibTeX
    Ref. manager
    Endnote
    DataCite
    NLM
    DC